Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 23, 2024 Local time: 02:19

Trump asema ataiwekea vikwazo Iraq iwapo vikosi vya Marekani vitafukuzwa


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Rais wa Marekani Donald Trump amesema Marekani haitaondoka Iraq mpaka itakapolipwa gharama iliyotumia kujenga kituo cha jeshi la anga katika nchi hiyo.

Trump alikuwa anajibu Jumapili azimio lililopitishwa na bunge la Iraqi linaloitaka serikali ya nchi hiyo kuamuru vikosi vya Marekani vyenye wanajeshi 5,200 kuondoka nchini humo.

Trump amewaambia waandishi akiwa ndani ya ndege ya Air Force One Jumapili usiku kuwa Marekani ina kituo cha jeshi la anga cha "gharama kubwa isiyo ya kawaida" nchini Iraq kilicho gharimu mabilioni ya dola za Marekani.

Kauli ya Bunge la Iraq kwa Jeshi la Marekani : ‘Ondokeni’

“Hatutaondoka mpaka watulipe gharama za ujenzi wa kambi hiyo,” amesema Trump, akitishia kuiwekea vikwazo Iraq “ambavyo hawajawahi kuvishuhudia” iwapo Marekani itashindwa kuondoka Iraq kwa “ msingi wa kirafiki zaidi.”

Serikali ya Marekani inatumia vituo 12 tofauti vya kijeshi vilivyoko Iraq. Trump hakupambanua ni kituo gani alichokuwa anakizungumzia.

Hatua ya Bunge la Iraqi kuvitaka vikosi vya Marekani kuondoka inatokana na maandamano dhidi ya kitendo cha Marekani kutumia ndege isiyokuwa na rubani kushambulia uwanja wa ndege wa Baghdad na kumuua jenerali wa ngazi ya juu wa Iran Qassem Soleimani.

Washia walio wengi katika bunge la Iraq walipiga kura kupitisha azimio hilo likitaka serikali ya mpito kusitisha mkataba wa pande mbili ambapo muungano wa jeshi linaloongozwa na Marekani liliweka vikosi vyake katika ardhi ya Iraq.

XS
SM
MD
LG