Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 06, 2022 Local time: 09:22

Trump aongeza muda wa serikali kuu kuchangia gharama za walinzi Louisiana


Rais Donald Trump atembelea maeneo yaliyoharibiwa na kimbunga Laura katika eneo la Ziwa Charles, Louisiana.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema katika taarifa yake Jumamosi usiku kuwa ataongeza muda wa serikali kuu kuchangia gharama za kuwepo kwa walinzi wa kitaifa huko Louisiana kuendelea kulisaidia jimbo hilo kukabiliana na COVID-19 na kuliwezesha jimbo hilo la Kusini kuufufua uchumi wake.

Idara zote za afya ya umma nchini Marekani zinakitaka kituo cha Marekani cha Kudhibiti na Kuzuia magonjwa (CDC) kusitisha mabadiliko yaliofanywa na serikali kuu hivi karibuni katika muogozo wa upimaji wa umma wa virusi vya corona.

Muungano wa Afya wa Miji Mikubwa na Jumuiya ya Kitaifa ya Kaunti na Maafisa Afya wa Miji, ambayo inawakilisha maelfu ya idara za maeneo, imetuma barua Ijumaa kwa wakuu wa CDC na Wizara ya Afya na Huduma za Binadamu zikiomba kubadili uamuzi uliotolewa wa kusimamisha upimaji wa watu waliokuwa wamekaribiana na virusi hivyo lakini hawaonyeshi dalili zozote za maambukizi.

Taasisi hizo zimeyataka mashirika ya serikali kurejesha mapendekezo yaliyotolewa hapo awali yanayotaka watu waliokaribiana na virusi hivyo wapimwe hata kama hawaonyeshi dalili zozote za maambukizi.

Majimbo yasiopungua 33 hayafuati miongozo mipya ya CDC na wanaendelea kupendekeza watu wote waliokaribiana na virusi vya corona wapimwe hata kama hawana dalili za maambukizi, kwa mujibu wa uchambuzi uliofanywa na shirika la habari la Reuters.

Chuo Kikuu cha Johns Hopkins nchini Marekani kinaripoti kuwa kuna zaidi ya maambukizi milioni 25 ya COVID-19 duniani. Marekani inakaribia kufikia maambukizi milioni 6, ikufuatiwa na Brazil yenye maambukizi milioni 3.8 na India maambukizi milioni 3.5.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG