Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 16:39

Tetemeko lenye nguvu laua zaidi ya watu 1,500 Uturuki na Syria


Zoezi la uokoaji likiendelea nchini Uturuki kufuatia tetemeko la ardhi, Jumatatu.
Zoezi la uokoaji likiendelea nchini Uturuki kufuatia tetemeko la ardhi, Jumatatu.

Tetemeko  la ardhi lenye ukubwa wa 7.8  kwa kipimo cha rikta lilitokea mapema Jumatatu na limeua zaidi ya watu 1,700 nchini  Uturuki na Syria na juhudi za kuwatafuta manusura zikiendelea katika vifusi vya majengo yalioanguka.

Tetemeko hilo lililotokea kabla ya alfajiri ambapo kitovu chake kilikuwa karibu na mji wa Gaziantep, karibu na mpaka wa Uturuki na Syria, lilifuatiwa na tetemeko jingine lenye ukubwa wa 7.5 kiasi cha kilomita 100 kaskazini mapema wakati wa mchana.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan aliuambia mkutano wa waandishi wa habari kuwa Uturuki ilirekodi vifo 912, na majeruhi 5,400. Alisema takriban majengo 2,800 yalianguka.

“Kwa sababu juhudi za kuondoa kifusi zinaendelea katika majengo mengi kwenye eneo la tetemeko, hatujajua ni kiwango gani cha vifo na majeruhi kitaongezeka,” Erdogan alisema.

Maafisa wa afya wa Syria walisema watu wasiopungua 371 wameuawa katika eneo linalodhibitiwa na serikali, waokoaji walisema watu wasiopungua 221 wengine walifariki katika maeneo yanayodhibitiwa wa waasi.

Wafanyakazi wa uwokozi na maafisa wa usalama wa Syria wakijaribu kuwatowa watu kutoka vifusi
Wafanyakazi wa uwokozi na maafisa wa usalama wa Syria wakijaribu kuwatowa watu kutoka vifusi

Tetemeko hilo la ardhi limeharibu jumba la kihistoria la Gaziantep Castle na majengo mengine ya kihistoria katika eneo hilo.

Katika mji wa Mersin, Uturuki, mkazi Nurhan Kiral ameiambia Sauti ya Amerika idhaa ya Uturuki kuwa tetemeko hilo lilidumu kwa dakika moja.

“Tuliamshwa na tetemeko na kutoka vitandani. Kifusi kilikuwa kinaanguka kutoka katika mlingoti wa kutoa moshi, na kifusi kilidondoka kutoka maeneo matupu kati ya majengo. Ilikuwa inatisha,” Kiral alisema.

Kundi la Syrian American Medical Society ilisema hospitali nchini Syria “zilikuwa zimeelemewa huku wagonjwa wakiwa wamefurika katika maeneo ya hospitali.

“Hospitali nyingi zimejaa, lakini baadhi ya vituo muhimu, ikiwa pamoja na hospitali ya Al Dana ilibidi wagonjwa waondolewe baada ya kupata uharibifu mkubwa kutokana tetemeko la ardhi,” kundi hilo lilisema katika taarifa yake. “Hivyo hivyo, hospitali ya wazazi ya Idleb ililazimika kuwapeleka watoto wachanga katika hospitali ya karibu.”

Wafanyakazi wa uwokozi na maafisa wa usalama wa Syria wanawatafuta watu walokwama ndani ya vifusi
Wafanyakazi wa uwokozi na maafisa wa usalama wa Syria wanawatafuta watu walokwama ndani ya vifusi

Umoja wa Ulaya ulisema umehamasisha timu za waokoaji katika eneo, wakiwemo wafanyakazi kutoka Bulgaria, Croatia, Jamhuri ya Czech, Ufaransa, Ugiriki, Hungary, Malta, Uholanzi, Poland na Romania.

“Mawazo yetu yako kwa wale ambao wamewapoteza wapendwa wao na mashujaa waliojitokeza kuokoa maisha ya watu,” mkuu wa sera za mambo ya nje wa EU Joseph Borrell na Kamishna wa Usimamizi wa Maafa Janez Lenarcic alisema katika taarifa ya pamoja.

XS
SM
MD
LG