Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 17, 2024 Local time: 18:57

Uturuki imefuta ziara ya Waziri wa Ulinzi wa Sweden


Waziri wa Ulinzi wa Uturuki, Hulusi Akar
Waziri wa Ulinzi wa Uturuki, Hulusi Akar

Waziri wa Ulinzi wa Uturuki, Hulusi Akar amesema hakuna sababu yoyote kwa ziara ya Waziri wa Ulinzi wa Sweden Pål Jonson ya Januari 27 kwa sababu Sweden haijachukua hatua zozote za kuzuia maandamano ya "kuchukiza" dhidi ya Uturuki nchini Sweden

Uturuki imefuta ziara iliyopangwa ya Waziri wa Ulinzi wa Sweden mjini Ankara kwa sababu nchi hiyo ya Nordic imetoa ruhusa kwa waandamanaji kufanya maandamano dhidi ya Uturuki nje ya ubalozi wa Uturuki mjini Stockholm.

Waziri wa Ulinzi wa Uturuki, Hulusi Akar amesema hakuna sababu yoyote kwa ziara ya Waziri wa Ulinzi wa Sweden Pål Jonson ya Januari 27 kwa sababu Sweden haijachukua hatua zozote za kuzuia maandamano ya "kuchukiza" dhidi ya Uturuki nchini Sweden.

Sweden inataka kuwa mwanachama wa NATO. Uturuki ambayo ni mwanachama wa NATO imezuia kuidhinisha azma ya Sweden kujiunga na muungano huo kwa sababu Sweden inaendelea kuruhusu maandamano. "Hatua zilipaswa kuchukuliwa," Akar alisema katika taarifa ya wizara ya ulinzi ya Uturuki.

Uturuki ilimuita balozi wa Sweden siku ya Ijumaa kutokana na maandamano yaliyopangwa kufanyika nchini Sweden na mpango wa kuchomwa kwa Quran wakati wa maandamano hayo.

XS
SM
MD
LG