Tetemeko hilo la kiwango cha 6.8 kwa kipimo cha rikta lilikuwa takriban kilomita 28 nje ya Herat, mji mkuu wa jimbo la Herat.
Kitovu cha tetemeko la Jumamosi lilikuwa maili 25 kaskazini magharibi mwa mji huo, na matetemeko mengine baada ya hapo yalifuatia.
Maafisa wa Taliban wamesema zaidi ya watu 2,000 wamekufa huko Herat baada ya matetemeko ya awali.
Kundi la misaada la madaktari wasio na mipaka limesema hospitali ya kanda ya Herat imepokea watu 117 waliojeruhiwa kutokana na tetemeko la leo.
Tetemeko la leo pia limeharibu nyumba 700 katika kijiji cha Chahak ambacho kilikuwa hakijawahi kukumbwa na tetemeko katika siku zilizopita.
Forum