Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 00:22

Uokozi unaendelea bada ya tetemeko la ardhi Afghanistan


Serikali ya Taliban, na mashirika ya misaada magharibi mwa Afghanistan, Jumatatu yamesema juhudi za uokoaji zinaendelea kuwatafuta na kuwaokoa walio nusurika na kukwama chini ya vifusi.

Siku mbili baada ya tetemeko kubwa la ardhi na mitetemeko mingi iliyofuata na kuua mamia ya watu na kujeruhi wengine wengi.

Tetemeko hilo la kipimo cha 6.3 lilitokea katika mkoa wa magharibi wa Herat, Jumamosi, na kuharibu zaidi ya vijiji kumi na mbili ndani na karibu ya wilaya ya Zinda Jan iliyoathirika zaidi. '

Maafisa na mashahidi walisema eneo la maafa lilitikiswa mara mbili na mitetemeko mipya Jumatatu, na kuukumba mji mkuu wa jimbo hilo, Herat, na kuwakimbiza maelfu ya wakaazi wake mitaani.

Wakati serikali ya Taliban imeripoti vifo vya takriban watu 2,000 tangu siku ya kwanza ya maafa Jumamosi, Umoja wa Mataifa umethibitisha vifo vya zaidi ya watu 1,000, na kusema kuwa karibu 1,700 walijeruhiwa.

Forum

XS
SM
MD
LG