“Baadhi tuna imani bado wapo chini ya vifusi,” alisema Matiul Haq Khalis, rais wa hilali nyekundu ya Afghanistan, baada ya kutembelea maeneo yaliyoathiriwa na tetemeko katika mkoa wa Herat, Jumanne.
Katika kijiji kilichopo katika kitovu cha tetemeko la ardhi, inaripotiwa kuwa takriban mauti 300 wamezikwa.
Wizara ya afya ya Afghanistan, imeripoti vifo 2,445 mpaka sasa, lakini ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu (OCHA) imetoa idadi ndogo ya vifo kuwa ni 1,300 na watu 500 hawajulikani walipo.
Forum