Zaidi ya nyumba 1,300 ziliporomoka wakati tetemeko la Jumamosi la kipimo cha 6.3 cha rikta-- likifuatiwa na mitetemeko minane mikubwa -- iliyotikisa maeneo ambayo ni magumu kufikia, takriban kilomita 30 kaskazini magharibi mwa mji mkuu wa mkoa wa Herat, kulingana na maafisa.
Katika wilaya ya vijijini ya Zinda Jan, kaya za vijiji zrundo la mawe na vifusi, ambapo timu za uokoaji za muda ziliendelea kuchimba katika juhudi za kuokoa watu na kuopoa mili siku ya Jumapili.
Misaada ilipelekwa taratibu katika eneo la janga hilo ikiwa ni pamoja na chakula, maji, mahema na majeneza.
Msemaji wa wizara ya usimamizi wa majanga Mullah Janan Sayeq alisema taifa hilo "lilishuhudia tetemeko la ardhi ambalo halijawahi kutokea," na kupelekea idadi ya waliofariki kuwa 2,053 katika vijiji 13 siku ya Jumapili.
Forum