Tetemeko hilo lilikuwa na ukubwa 6.3 kwenye vipimo vya rikta, taasisi ya Marekani ya utafiti wa kijeolojia ilisema, huku mitetemeko iliyofuata ikipiga kilomita 35 kaskazini magharibi mwa mji wa Herat.
Takwimu hizo za vifo ni za ripoti ya awali kutoka wilaya ya Zinda Jan ya jimbo la Herat, msemaji wa wizara ya usimamizi wa majanga Jan Sayeq alisema.
Aliongeza kuwa mitetemeko hiyo ilitikisa pia majimbo ya Farah na Badghis, ambako kumeripotiwa uharibifu mkubwa wa nyumba, lakini hakuna maelezo yaliyotolewa kuhusu vifo.
Forum