Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 26, 2022 Local time: 12:47

Tanzania : Chadema yadai vipo viashiria jeshi la polisi linajitumbukiza katika siasa


John Mnyika

Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema kimelitaka jeshi la polisi nchini humo kujiweka kando na masuala ya kisiasa ili kuacha uwanja wa kisiasa kuwa sawa kwa vyama kushindana wakati huu wa kuelekea katika uchaguzi mkuu.

Ingawa chama hicho hakikubainisha moja kwa moja namna jeshi hilo linavyojitumbukiza katika masuala ya kisiasa. lakini kimesisitiza kwa kunukuu baadhi ya kauli zinazotolewa na maafisa wa jeshi hilo ambazo kimedai kwamba zinafanana na zile zilizowahi kutolewa na chama tawala ccm,

Akibainisha msimamo wa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu, katibu mkuu John Mnyika amedai kwamba usawa katika masuala yanayohusu uchaguzi ni mambo yanapaswa kuzingatiwa na pande zote zinazoshiriki uchaguzi huo.

Chama hicho ambacho karibuni kilitangaza majina ya wagombea 11 waliojitokeza kuwania nafasi ya urais wamedai kuwepo kwa viashiria kwamba jeshi la polisi linajitumbukiza katika masuala ya kisiasa na hivyo kufanya uwanja wa kisiasa kushindwa kutoa uwiano sawa kwa washiriki wa uchaguzi mkuu kuchuana kwa hoja na sera.

Mbali na kubainisha hayo chama hicho ambacho katika miezi ya hivi karibuni kimeshuhudia baadhi ya wabunge wake na madiwani wakikipa mkono wa kwaheri na kujiunga na chama tawala na vyama vinginevyo vya upinzani kimerejea hoja yake ya kutaka tume huru ya uchaguzi,

Kimesema ingawa kinaamini kinaingia katika uchaguzi huku hoja zao za kutaka tume huru ikiwa bado hazijapatiwa ufumbuzi, hata hivyo kipo tayari kwa uchaguzi huo.

Katika hatua nyingine chama hicho kimesisitiza kwamba mwenyekiti wake Freeman Mbowe alishambuliwa kisiasa huku kikipuuza taarifa zinazotolewa kwamba kiongozi huyo hakufanyiwa shambulizi lolote zaidi ya kukutwa akiwa amepata kilevi.

Mnyika : "Sasa kama mgonjwa zinatolewa taarifa za uongo dhidi yake, madaktari waliompokea mwenyekiti mara ya kwanza kabisa wajitokeze wasema waziwazi. Ukweli ni kwamba mwenyekiti hakuwa amelewa chakari kama ambavyo inavyosemwa, yote haya yanasemwa ili kuhamisha mjadala.

"Vitolewe vipimo kwa sababu tunajua kwamba hili jambo halipo ni bongo ni uzushi. Hatuna imani na uchunguzi ambar unaendelea kufanywa na jesti la polisi. Na chama kinaendelea kutafakari hatua za ziada za kuchukuwa. Lakini katika hatua hii kwa sasa tungependa wananchi wapuuze," amesema Mnyika.

Chadema inseam kiongozi huyo amefanyiwa upasuaji katika sehemu yake mguu na sasa anaendelea vyema yeye ni miongoni mwa wanachama 11 waliojitokeza kuomba nafasi ya kuwania uraisi.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG