Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 17:07

Tanzania : Spika Ndugai akosoa hotuba ya Chadema juu ya janga la corona


Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amekosoa vikali hotuba iliyotolewa na chama cha upinzani Chadema akisema kiongozi huyo amekuwa na ajenda isiyotaka kuitendea haki Tanzania hasa katika kipindi hiki cha janga la corona.

Spika Ndugai

Spika amesema kiongozi huyo wa kambi ya upinzani bungeni Freeman Mbowe kwanza amekuwa mtoro kuhudhuria vikao vya bunge na pia amekuwa akitoa shutuma zisizo na ukweli wowote.

“Ajifunze kubadilika Freeman Mbowe, amekuwa kiongozi muda mrefu, usiwapelekeshe wabunge wako kiasi hicho. Wabunge wakipata mshahara wanakatwa kupelekwa kwenye chama chake. Matumizi ambayo wala hayaeleweki. Waliniambia mimi ndio Spika wao. Situngi maneno. Kwa nini mnachukuwa fedha za wabunge hawa? Piga hesabu ya miaka 5 uone. Ni bilioni kadhaa. Zikisha fika hakuna transparency yoyote. Wanatumia wanavyotaka. Huwezi kuwa kiongozi namna hiyo. Jirekebishe na kusema wenzako. Na sisi lazima tukwambie maneno ambayo lazima urekebike.,” amekosoa Spika.

Freeman Mbowe
Freeman Mbowe

Mwenyekiti Mbowe

Katika mkutano wake Jumapili Mwenyekiti huyo wa Chadema Freeman Mbowe aliikosoa vikali serikali na kulishutumu bunge kwa namna linavyo shughulikia janga la corona.

Katika hotuba iliyopangwa tangu awali Mwenyekiti wa chama cha upinzani cha Chadema, Freeman Mbowe alijibu baadhi ya hoja za Rais Magufuli na kusema njia inayotumiwa na Tanzania katika kupambana na Covid-19 inaiweka nchi hiyo katika hatari.

Bila kutoa takwimu Mbowe alisema Tanzania bado inakabiliwa vikali na ugonjwa Covid-19. Aliongeza kuwa serikali ya Tanzania ingali na nafasi ya kuchukua baadhi ya hatua zaidi hata kwa kiwango kidogo ili kukabiliana na janga hilo badala ya kuficha ukweli.

Mbowe alitoa rai rasmi kwa Rais Magufuli akimsihi kwamba washauri wake wanamwogopa na hawamuelezi hali halisi ya ugonjwa huo nchini Tanzania.

Kiongozi huyu amesema kuweko kwa taarifa za nchi jirani kufunga mipaka na hata kuzuia Watanzania kuingia katika nchi hizo au kuwekewa utaratibu mpya wa masharti inatokana na kukataa ushauri wa kisayansi.

Siku za nyuma niliwahi kutoa tahadhari tusipokubali kufanya amri ya kutotoka nje hata ikiwa ni sehemu tu ya amri hiyo tutatengwa.

Amesema "mwanzoni tulizungumza kujifunza kutoka uzoefu wa nchi nyingine katika kupambana na janga la corona, sasa tunazungumzwa na nchi nyingine kama kielelezo hasi cha vita dhidi ya janga la corona Afrika na duniani.

Posho

Wakati huo huo Spika amemtaka kiongozi huyo kurejesha fedha alizopewa ambazo zilitolewa kama sehemu ya wabunge wanaohudhuria vikao vya bunge lakini pamoja na baadhi ya wabunge wenzake walisusia vikao hivyo.

“Fedha ambayo hukustahili kuichukua rudisha, usitafute visingizio ninafuatwa, ninasemwa, ungekuwa umerudisha ungesemwa? Unapaswa kurudisha mara moja.

Na kitendo cha kwamba mpaka leo tarehe 18, unaendelea mgomo wako. Sasa bado hivi naongea na nyinyi hajarudisha fedha, kuonyesha kwamba alikuwa na nia ya kuchukuwa hizo fedha kwa hiyo arudishe hizo fedha, hilo ni jambo la haraka.

Spika : “Waandishi na hakika hizo fedha zitarudi. Hilo wala msiwe na wasiwasi. Njia gani nitatumia nyie wala msiwe na wasiwasi. Hilo niachieni mimi na hakika, kwamba hizo fedha za umma zitarudi. Kwa upande huo ataniona mbaya bure. Ili tuelewane basi arudishe fedha hizo na awashauri wenzake ambao bado hawajarudisha warudishe fedha hizo. Na wengi wao wamekwisha kurudisha.”

Amesema mwanasiasa huyo amekuwa akitumia janga la kama kigezo cha kuisema serikali jambo ambalo amesisitiza kwamba halikubaliki hata kidogo.

Ndugai amuonya Mbowe

Freeman Mbowe ukimdharau rais wetu umetudharau sisi wote, kufanya kazi na sisi itakuwa vigumu sana. Yule ndio mkuu wa nchi. Jiepushe sana njia hizo unazoziendea, kwa sababu hazikusaidii. Anasema nchi hii uchumi umeharibika, umekwisha kwanza kwa sababu watalii hawaji hapa, kwenye hotuba yake.

Hivi nyinyi watalii siku hizi wanakwenda nchi gani? Wanaenda nchi gani? Hizo nchi jirani mtalii gani anakwenda wapi? Huko Rwanda anakosifia kuna mtalii anayekwenda? Huko Uganda kuna mtalii, Kenya kuna mtalii? Wapi kuna utalii? Unaponda nchi yako bila sababu yoyote. Na hii ni pandemic ni tatizo la dunia. Halikuletwa na mtu. Na kubeba nongwa kila wakati, kuzungumzia kana kwamba kuna jambo limeletwa na kundi fulani. Sijambo ambalo ni sawasawa.

XS
SM
MD
LG