Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 25, 2020 Local time: 02:37

Spika Ndugai apiga marufuku kucha, kope bandia bungeni


Bunge la Tanzania

Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai amepiga marufuku wabunge wanawake kuingia katika bunge wakiwa na kucha na kope bandia.

Spika huyo amesema hayo Jumatatu wakati wa kikao cha bunge Dodoma.

“Kwa mamlaka niliyopewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivi sasa napiga marufuku wabunge wote wenye kope na kucha bandia kuingia Bungeni,” Ndugai amesema.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, Tanzania, Spika ameongeza kuwa anashauriana na wataalamu kabla ya kufanya uamuzi iwapo aruhusu au asiruhusu wabunge wanaotumia vipodozi kupita kiasi kuingia katika Bunge.

Tangazo hilo limekuja muda mfupi baada ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr Faustine Ndugulile kuliambia Bunge kuwa wanawake wanaotumia kucha na kope bandia wanakabiliwa na hatarisho kubwa la kiafya ambalo linaigharimu taifa.

Kwa mujibu wa ripoti za afya zilizo thibitishwa, sio chini ya wanawake 700 wanalazwa hospitali nchini Tanzania wakiwa wanasumbuliwa na athari za kutumia kope na makucha bandia na kujichubuwa.

Facebook Forum

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG