Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 08:50

Chadema imeanza mchakato wa kuwatoa gerezani viongozi wake


Viongozi wa Chadema wakiwa mahakamani.
Viongozi wa Chadema wakiwa mahakamani.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeanza mchakato wa kuwalipia faini wabunge wa Kawe, Halima Mdee; Esther Matiko (Tarime Mjini) na Ester Bulaya(Bunda).

Vyanzo vya habari nchini Tanzania vimemnukuu mkurugenzi wa itikadi, uenezi, mawasiliano na mambo ya nje wa Chadema, John Mrema amesema mawakili wa chama hicho wameanza kufuatilia namba ili kulipa faini ya Shilingi 110 milioni inayotakiwa kulipwa na wabunge hao watatu ili watoke gerezani.

Viongozi wanane wa Chadema pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt Vicent Mashinji Machi 10, 2020 walihukumiwa kulipa fiaini ya Sh350 milioni au kwenda jela miezi mitano baada ya kutiwa hatiani kwa makosa 12 kati ya 13 yaliyokuwa yanawakabili.

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeeleza kuwa tayari kimemlipia mwanachama wake mpya Dkt Mashinji faini hiyo.

Washtakiwa hao wakiongozwa na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe walilazimika kwenda jela baada ya kushindwa kukamilisha taratibu za kulipa faini hiyo waliohukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Baada ya hukumu hiyo iliyosomwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, Chadema walianza kuchangishana fedha kwa ajili ya kuwalipia faini viongozi wake hao.

XS
SM
MD
LG