Uvamizi huo wa usiku kucha ulikuja saa kadhaa baada ya shambulizi la bomu nje ya msikiti mkuu wa Eid Gah Jumapili na kuua raia wa Afghanistan wasiopungua wanane, na kuwajeruhi wengine 20.
Hata hivyo hakuna aliyedai kuhusika na shambulizi hilo la kwenye msikiti.
Taliban hawakusema operesheni yao dhidi ya kikundi cha Afghanistan chenye mahusiano na Islamic State maarufu kama ISIS-K ilikuwa majibu ya mlipuko wa bomu uliosababisha vifo kwenye msikiti.
Kituo cha Daesh kiliharibiwa kabisa na wanachama wote wa Daesh waliokuwa ndani waliuawa kutokana na matokeo ya operesheni yenye mafanikio iliyofanywa vikosi maalum vya Taliban, Zabihullah Mujahid, msemaji mkuu wa Taliban alitangaza mapema leo.