Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 05, 2024 Local time: 15:11

Ndege ya Pakistan yatua Kabul


Ndege ya shirika la kimataifa la Ndege la Pakistan (PIA) ikiwasili uwanja wa ndege wa Kabul.
Ndege ya shirika la kimataifa la Ndege la Pakistan (PIA) ikiwasili uwanja wa ndege wa Kabul.

Ndege ya shirika la kimataifa la Ndege la Pakistan (PIA) kutoka Islamabad imetua mjini Kabul Jumatatu, msemaji wa shirika hilo alisema.

Ndege ya shirika la ndege la serikali ya Pakistani itabeba watu kutoka Kabul hadi Islamabad wenye hati halali za kusafiri.

Hata hivyo haijajulikana mara moja ikiwa imewekwa kama ndege ya kawaida ya kibiashara au kwa ajili ya safari maalum ya kibiashara.

Hii ni ndege ya kwanza ya PIA kutua mjini Kabul tangu kumalizika kwa uondoaji wa vikosi vya kigeni na idadi kubwa ya watu kutoka Afghanistan mapema mwezi huu.

XS
SM
MD
LG