Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 02, 2023 Local time: 18:13

Raia kadhaa wauawa katika mlipuko wa bomu Kabul


Wafanyakazi wa hospitali mjini Kabul wakisubiri kupokea wahanga waliouawa katika mlipuko wa bomu Oct. 3, 2021.(Photo by Hoshang HASHIMI / AFP)

Bomu limelipuka karibu na mlango wa kuingilia msikitini katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, na kuua “raia kadhaa,” msemaji wa Taliban amesema Jumapili.

Watu walikuwa wamekusanyika katika msikiti wa Eidgah kumuombea marehemu mama yake msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid aliyefariki hivi karibuni.

Hakuna aliyedai kuhusika na mlipuko wa bomu hilo.

Wakati Taliban walipochukua madaraka nchini humo katikati ya mwezi Agosti, mashambulizi yanayo fanywa na washirika wa Islamic State yameongezeka.

IS inakadiriwa kuwa ni adui wa Taliban.

Chanzo cha habari ni VOA na shirika la habari la AP.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG