Rais Omar al Bashir afanya ziara ya kihistoria Sudan Kusini ikiwa ni ya kwanza tangu nchi hizo mbili kutengana 2011.
Rais Omar al-Bashir atembelea Sudan Kusini
1
Rais Salva Kiir (kulia) akimsalimia mgeni wake wa Sudan Omar al Bashir alipowasili uwanja wa ndege wa Juba, Ijuma, Aprili 12, 2013.
2
Ndege ya rais Omar al Bashir ikiwasili kwa ziara ya kwanza Sudan Kusini ikiwa imetuwa kwenye uwanja wa ndege wa Juba Ijuma, Aprili 12, 2013.
3
Bendi ya jeshi la Sudan Kusini linamkaribisha rais wa Sudan Omar al Bashir mjini Juba.
4
Marais wa Sudan na Sudan Kusini wakisimama pamoja wakati wimbo wa taifa unapigwa wa nchi zote mbili kwenye uwanja wa ndege wa Juba, Aprili 12, 2013.