Shirika la habari lenye uhusiano na serikali ya Ethiopia, FANA, limeripoti kwamba waziri wa elimu Berhanu Nega amesema kwamba shule zitafungwa kwa muda wa wiki moja.
Serikali ilisema Jumatatu kwamba zaidi ya wanafunzi milioni 1.2 hawapo shule kutokana na mapigano yanayoendelea kaskazini mwa nchi hiyo.
Mapigano yameharibu mamia ya shule.
Serikali ilitangaza hali ya dharura ya miezi sita kuanzia mwezi Novemba ili kukabiliana na wapiganaji wa Tigray wenye lengo la kuingia mji mkuu wa Addis Ababa na kuuangusha utawala wa waziri mkuu Abiy Ahmed.