Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 19, 2024 Local time: 17:49

Waziri Mkuu wa Ethiopia ayataka majeshi kuwaangamiza maadui


Waziri Mkuu Abiy Ahmed
Waziri Mkuu Abiy Ahmed

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema maadui zake wameshindwa na kuahidi kulikamata tena eneo katika mkoa wa Amhara kutoka kwa wapiganaji wa Tigray

Amesema hayo wakati akipongeza ushindi wa jeshi dhidi ya wapiganaji waTigray kwenye eneo la Afar.

Picha kutoka mstari wa mbele zilizorushwa na shirika la utangazaji – FANA siku ya Jumanne zilimuonyesha Abiy akiwa amevalia sare za kijeshi na kofia akitazama kwa kutumia darubini.

Fana imesema Abiy alikuwa akitoa maelekezo kwa wanajeshi walioko mstari wa mbele kwenye mzozo wa Ethiopia karibu na eneo la Gashena kwenye mkoa wa Amhara, Shirika la habari la ROITA limethibitisha.

Abiy ambaye vikosi vyake vimekuwa vikipambana kutoka mkoa wa kaskazini wa Tigray kwa zaidi ya mwaka mmoja akisema kuwa anaelekea mstari wa mbele kuongoza operesheni za mapambano.

Vyombo vya habari vya serikali vimeripoti mwishoni mwa wiki kwamba jeshi limekamata mji wa chifra kwenye mkoa wa Safar na maeneo mengine, baada ya Abiy kuwasili.

XS
SM
MD
LG