Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 08:05

Abiy yuko mstari wa mbele vita dhidi ya TPLF


Wanajeshi wa Ethiopia wakipiga doria karibu na Agula, kaskazini mwa Mekele, eneo la Tigray, kaskazini mwa Ethiopia, May 8, 2021.
Wanajeshi wa Ethiopia wakipiga doria karibu na Agula, kaskazini mwa Mekele, eneo la Tigray, kaskazini mwa Ethiopia, May 8, 2021.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, amesema Ijuma kwamba “watawazika maadui”, akitoa ujumbe wake wa kwanza tangu kuwasili kwenye mstari wa mbele wa vita, kati ya jeshi la serikali na wapiganaji wa kundi la ukombozi wa tigray TPLF.

Video iliyochapishwa kwenye ukurasa wa twitter wa Abiy hii leo, inamonesha kiongozi huyo akiwa pamoja na viongozi wa jeshi katika êneo la mstari wa mebele wa vita.

Katika mahojiano na televisheni ya Fana, Abiy ameonekana akiwa amevalia sare za kijeshi, Akizungumza katika lugha za Afaan Oromo na Amharic.

Amesema “Unachoona huko ni mlima ambao ulikuwa umedhibitiwa na maadui kufikia jana. Sasa tumefanikiwa kuudhibithi”.

Ameendelea kusema kwamba “ari ya adui imeanza kupungua," na kuahidi kwamba wanajeshi wa serikali watauteka mji wa Chifra ulio mpakani na Tigray na Afar, kufikia “leo”.

“Hatutarudi nyuma hadi tuwazike maadui na kuhakikisha kwamba Ethiopia ipo huru. Tunachotaka kuona ni Ethiopia inayoweza kujisimamisha, na tutakufa tukipigania hilo,” amesema Abiy.

Jumuiya ya kimataifa imeshitushwa na uwamuzi wa Abiy kuelekea kwenye mstari wa mbele wa mapigano, ikitoa wito wa kusitisha mara moja mapigano na kutafuta suluhisho kwa njia ya mazungumzo.

Abiy alitangaza Jumatatu usiku kwamba alikuwa anaelekea msitari wa mbele wa jeshi la Ethiopia, katika vita dhidi ya wapiganaji wa TPLF na washirika wao.

Wapiganaji wa Tigray wametishia kuingia mji mkuu wa Addis Ababa au kujaribu kukata mawasiliano kati ya bandari kubwa eneo hilo na Ethiopia.

Mjumbe maalum wa Marekani kwa ajili ya Ethiopia Jeffrey Feltman, amesema wiki hii kwamba wapiganaji wa Tigray wamesonga mbele pande za kusini wakielekea mji mkuu lakini jeshi la Ethiopia limetekeleza mashambulizi mara kadhaa na kuzuia jaribio lao la kudhibithi njia kuu ya kuelekea bandari iliyo mashariki.

Zaidi ya watu milioni 9.4 wanahitaji msaada wa chakula kutokana na vita hivyo vya karibu mwaka mmoja.

XS
SM
MD
LG