Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 12:53

Hatuhusiki na shambulizi kwenye mpaka na Sudan. Ni wapiganani wa Tigray - Serikali ya Ethiopia


Ethiopia imekanusha kuwa ilifanya shambulio mwishoni mwa juma kwenye mkapa wake na Sudan, ikiwashtumu waasi wa Tigray kuchochea mzozo huo.

Jumamosi, jeshi la Sudan lilisema wanajeshi kadhaa waliuawa katika shambulio lililofanywa na makundi yenye silaha na wanamgambo wenye uhusiano na jeshi la Ethiopia katika jimbo la Al Fashaqa.

Jimbo hilo limekuwa tangu zamani chanzo cha mvutano kati ya Addis Ababa na Khartoum, na kusababisha mapambano makali mwaka uliopita.

Lakini katika maelezo yaliyopeperushwa kwenye chombo cha habari cha serikali jana Jumapili, msemaji wa serikali ya Ethiopia Legesse Tulu amekanusha madai kwamba jeshi la Ethiopia lilishambulia Sudan, akisema madai hayo hayana msingi.

Badala yake, amewashtumu wapiganaji wa chama cha Tigray People”s Liberation Front (TPLF) kuchochea ghasia hizo. TPLF iko katika vita na serikali ya waziri mkuu Abiy Ahmed tangu Novemba mwaka jana, TPLF imedai kwamba iko karibu na mji mkuu Addis Ababa.

Legesse alisema kundi kubwa la waasi, majambazi na magaidi lililingia kutoka Sudan, bila kutoa ushahidi.

Aliongeza kuwa jeshi la Ethiopia na kwa ushirikiano na wanamgambo walitokomeza waasi hao.

XS
SM
MD
LG