Mwanafunzi wa mwaka wa pili mwenye umri wa miaka 15 alifyatua risasi katika shule anayosoma kwenye jimbo la Michigan siku ya Jumanne na kuwauwa wanafunzi watatu akiwemo mvulana mwenye umri wa miaka 16 aliyefariki kwenye gari la maafisa wa doria akiwa njiani kupelekwa hospitali, mamlaka zimesema.
Watu wengine wanne walijeruhiwa baadhi yao wakiwa katika hali mbali. Afisa wa polisi wa kaunti ya Okland, Michael Bouchard, amesema jana jioni kwamba wachunguzi bado wanafanya upepelezi kugundua sababu ya shambulizi hilo la risasi katika shule ya sekondari ya Oxford, kwenye eneo ambalo lina watu takriban 22,000.
“ Kama nilivyosema, tunaye mtuhumiwa chini ya ulinzi . Ni mvulana mwenye umri wa miaka 15, mkazi wa kijiji cha Oxford. Hakujeruhiwa na hivi sasa yuko katika kituo cha watoto hapa kufuatia mauaji hayo na jaribio la kuuwa, anashikiliwa kwa idhini ya mahakama.
Amesema : "Hatuwezi kumtambulisha kwa wakati huu kwa sababu yeye ni kijana mdogo na hajashtakiwa kama mtu mzima. Kwa hiyo hakuna uwezo wa kumtambua kwa wakati huu. Pamoja na wazazi wake kuwepo alikataa kuzungumza na wameajiri mwanasheria.” Shule ilifungwa baada ya shambulizi hilo.