Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 08:21

Wanafunzi 7 wauawa katika shambulizi la bunduki nchini Russia


Ambulensi na malori yaliyoegeshwa kwenye lango la shule ambako shambulizi lilioua wanafunzi wasiopungua saba lilitokea nchini Russia tarehe 11, Mei, 2021.
Ambulensi na malori yaliyoegeshwa kwenye lango la shule ambako shambulizi lilioua wanafunzi wasiopungua saba lilitokea nchini Russia tarehe 11, Mei, 2021.

Wanafunzi 7 waliuawa Jumanne na wengine wengi kujeruhiwa baada ya mwanafunzi mwenzao kufyatua risasi kwenye shule moja mjini Kazan nchini Russia, mkuu wa mkoa amesema.

Akilitaja shambulizi hilo kuwa janga kubwa kwa nchi nzima, mkuu wa mkoa wa Tatarstan Rustam Minnikhanov alisema kuwa hakuna ushahidi kwamba kuna mtu mwengine yeyote aliyehusika katika shambulizi hilo.

“Tumepoteza watu 7, wavulana wanne na wasichana wa tatu. Watu 16, watoto 12 na watu wazima wanne wamelazwa hospitali," Minnikhanov aliiambia televisheni ya serekali ;

Aliongeza kuwa mshambuliaji alikamatwa nba kwamba ni kijana wa miaka 19 ambae aliorodheshwa mmiiliki rasmi wa silaha.

Kuna uwezekano idadi ya waliouwawa ikaongezeka. Mapema, vyombo vya habari vya Russia vikinukuu chanzo cha wizara ya afya, vimesema watu 11 walifariki katika shambulizi hilo.

Kazan ni mji mkuu wa mkoa wa Tatarstan unaokaliwa na waislamu wengi, ambao uko umbali wa kilomita 725 mashariki mwa Moscow.

Mashambulizi ya ufyatuaji risasi shuleni ni nadra nchini Russia. Shambulizi kubwa la kipekee lilitokea katika eneo lililozingirwa na Russia la Crimea mwaka 2018, ambapo mwanafunzi wa chuo kikuu aliuwa watu 19 kabla ya kujiua mwenyewe

-Imetayarishwa na Patrick Nduwimana, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG