Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 07, 2022 Local time: 19:09

Watu watatu Wafariki katika mashambulizi ya risasi huko Austin, Texas


Polisi katika eneo la tukio la upigaji risasi huko Austin, Texas.

Watu wasiopungua watatu waliuawa Jumapili kwa kupigwa risasi huko Austin, Texas, katika jengo la makazi ya watu mamlaka zilieza.

Polisi wa Austin, waliita hali hiyo tukio la upigaji risasi linaloendelea na walisema walikuwa wakimtafuta mtuhumiwa.

Wakati mtuhumiwa hajulikani alipo, inaonekana hii ni hali ya shambulizi la ndani ambalo ni la kipekee na hakuna hatari kwa umma kwa ujumla, polisi wa Austin walisema kwenye Twitter.

Upigaji risasi ulitokea karibu na eneo maarufu la Maduka Kaskazini magharibi mwa jiji, ambalo ni mji mkuu wa Texas.

Polisi wanajua utambulisho wa mtu mwenye bunduki, kulingana na ripoti ya KVUE-TV huko Austin.

Idara ya Huduma za Matibabu ya Dharura ya Kaunti ya Austin-Travis ilisema watu wazima watatu walikuwa wamekufa katika eneo la tukio, ambalo liliripotiwa muda mfupi kabla ya saa sita, mchana saa za huko.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG