Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 05:29

Seneta Collins atangaza kumpigia kura Kavanaugh


Jaji Brett Kavanaugh
Jaji Brett Kavanaugh

Seneta Susan Collins wa Marekani, Mrepublikan ambaye anachukuliwa kuwa mwenye kura ya kubadilisha matokeo kati ya wawakilishi watakao amua uteuzi wa Jaji Brett Kavanaugh kuingia Mahakama ya Juu Marekani, ametangaza kuwa atampigia kura mteule huyu.

Kura ya kumthibitisha Jaji Kavanaugh inaweza kupigwa mapema Jumamosi.

Collins amesema kukosekana ushahidi kwa tuhuma dhidi ya Kavanaugh ndio sababu ya kumuunga mkono. Lakini ameongeza kuwa uamuzi wake isichukuliwe kwamba anakanusha umuhimu wa madai ya unyanyasaji wa kingono.

“Kila mtu au mwanamke ambaye anashtaki juu ya udhalilishaji wa kingono anahaki ya kusikilizwa na kuwekewa heshima yake,” amesema.

Kura ya Collins ya ndiyo inafanya kuthibitishwa kwa Kavanaugh kuwa na uwezekano mkubwa. Iwapo kura ya Seneta Mdemokrat Joe Manchin pekee, ambaye mpaka sasa hajaamua kumpigia, iwapo atampigia kura ya ndiyo, itafanya Kavanaugh athibitishwe kwa hisabu ya kura 51-50.

Iwapo Manchin atapiga kura ya hapana, na Baraza la Seneti litakuwa na kura zilizofungana 50-50, Makamu wa Rais Mike Pence atapiga kura ya kumpitisha mteule huyo kwa kuongeza hisabu ya kura ya upande moja.

Kavanaugh anatuhumiwa kwa udhalilishaji wa kingono na mwanamke ambaye anasema alimkabili katika nyumba moja iliyoko katika kitongoji cha Washington wakati wakiwa ni vijana miaka ya 1980.

Lakini mteule huyo amekanusha tuhuma hizo zilizo tolewa na Profesa Christine Blasey Ford, aliyetoa ushahidi mbele ya Kamati ya Sheria ya Seneti kiasi ya zaidi ya wiki iliyopita.

XS
SM
MD
LG