Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 25, 2025 Local time: 14:48

Hatma ya mteule wa Trump kujulikana Ijumaa


Profesa Ford (Kulia), Jaji Kavanaugh (Kushoto)
Profesa Ford (Kulia), Jaji Kavanaugh (Kushoto)

Kamati ya Sheria ya Baraza la Seneti itapiga kura Ijumaa asubuhi juu ya uteuzi wa Brett Kavanaugh kuingia Mahakama ya Juu, kufuatia siku moja ya mahojiano yaliyo mhusisha jaji wa mahakama ya rufani na Christine Blasey Ford anaye mtuhumu jaji huyo kwa kumdhalilisha kingono.

Warepublikan 11 na Wademokrat 10 katika kamati hiyo wataamua iwapo wamthibitishe Kavanaugh ili apitishwe na Baraza lote la Seneti, ambalo linatarajiwa kuanza utaratibu wa kupiga kura Jumamosi..

Chama cha Wanasheria wa Marekani Alhamisi jioni kilihimiza kuwa Kamati ya Sheria na Baraza kamili la Seneti licheleweshe kupiga kura mpaka pale Shirika la Upelelezi wa Makosa ya Jinai ( FBI ) lipewe fursa kufanya uchunguzi wa kina wa maisha ya jaji juu ya madai yaliyotolewa na Ford na wanawake wengine.

“Tunatoa pendekezo hili kwa sababu ya sisi kama ABA tunavyo heshimu utawala wa sheria na kufuata mchakato unaostahili chini ya sheria,” barua ya ABA iliyo tumwa kwa uongozi wa kamati imesema. Kila mteule ambaye anatakiwa kushikilia nafasi ya juu kabisa ya mahakama (kama ilivyo na wateule wengine wote) kwa kifupi ni muhimu sana na haistahili kukimbilia kupiga kura.”

Haiko wazi iwapo Warepublikan watapata kura za kutosha kwa ajili ya mteule wao baada ya mahojiano yaliyo kuwa na hisia za juu Alhamisi wakati Kavanaugh kwa hasira akikanusha tuhuma za kumdhalilisha kingono Ford katika tafrija mwaka 1982, wakati wakiwa vijana. Wote wawili walitoa maelezo yao kwa Kamati ya Sheria ya Baraza la Seneti katika mahojiano yaliyo chukua masaa tisa.

Alhamisi jioni, Seneta Bob Corker wa Jimbo la Tennessee alitangaza kuwa atampigia kura kuthibitisha Kavanaugh katika uteuzi huo wa Mahakama ya Juu. Wakati huohuo, amesema, ilikuwa ni ushujaa mkubwa kwa Ford kutoa ushahidi, kwani kulikuwa hakuna ushahidi wa kuthibitisha madai yake.

Seneta Jeff Flake wa Arizona amesema bado anafikiria namna ya kupiga kura baada ya kusikia maelezo ya Ford na Kavanaugh.

Alipoulizwa atampigia kura nani, Flake alisema “Niache nilifikirie hilo.”

Seneta Heidi Heitkamp, Mdemokrati kutoka jimbo la North Dakota, pia amesema anahitaji muda kufanya uamuzi juu ya kura yake. Anagombania kuchaguliwa tena katika jimbo ambalo lilimchagua kwa kura nyingi Rais Donald Trump.
Seneta Doug Jones wa Alabama, ambaye anatumikia awamu yake ya kwanza, amesema anapiga kura kupinga uteuzi wa Kavanaugh kuingia Mahakama ya Juu. “Mchakato wa uteuzi wa Kavanaugh umekabiliwa na kasoro tangia mwanzo,” amesema, akiongeza kuwa Ford ni shupavu na mkweli.

XS
SM
MD
LG