Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 08:31

Ford akubali kutoa ushahidi mbele ya Seneti


Jengo la bunge la Marekani
Jengo la bunge la Marekani

Dkt Christine Blazey Ford na mwanasheria wake wamekubali kutoa ushahidi mbele ya Baraza la Seneti la Marekani wakiomba vyombo vya habari visiwepo ndani ya chumba cha utoaji ushahidi na pia Kavanaugh asiwepo.

Kamati ya Sheria ya baraza hilo na mawakili wake Ford ambaye anamshutumu Brett Kavanaugh mteuliwa katika nafasi ya Mahakama ya Juu, Marekani, kwa kumshambulia kingono wakati wawili hao wakiwa shule ya sekondari, wamefikia makubaliano kwamba atatoa ushahidi mbele ya kamati hiyo Alhamis wiki ijayo.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari pande hizo mbili zilifikia makubaliano kwa njia ya simu Jumamosi na wanatarajiwa kuzungumzia vipengele vya sheria kuhusu kutokea kwa Christine Blasey Ford mbele ya kamati hiyo.

Hata hivyo haijafahamika iwapo maombi ya Ford ya kutokuwepo vyombo vya habari yamekubaliwa au la.

Lindsey Graham
Lindsey Graham

Seneta Mrepublikan Linsey Graham alikiambia kituo cha televisheni cha Fox News cha Marekani “Ford atapatiwa huduma sawa lakini hatutaelekeza maswali kwa mawakili wake”.

XS
SM
MD
LG