Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 09, 2022 Local time: 22:25

Uteuzi wa Kavanaugh : Kura kamili baada ya upelelezi wa FBI


Jaji Kavanaugh

Kamati ya Sheria ya Baraza la Seneti imepiga kura kwa kuzingatia msimamo wa vyama Ijumaa ili kupeleka mbele uteuzi wa mteule wa Mahakama ya Juu Brett Kavanaugh kwenda kwenye Baraza kamili la Seneti, ingawaje inaomba wiki moja kulipa nafasi shirika la Upelelezi wa Makosa ya Jinai (FBI) kufanya uchunguzi.

Hili linajiri siku moja baada ya mahojiano yaliyo mhusisha jaji wa mahakama ya rufani na Christine Blasey Ford anaye mtuhumu jaji huyo kwa kumdhalilisha kingono.

Nafasi ya Kavanaugh kuthibitishwa iliongezeka wakati Seneta Jeff Flake wa Republikan, mwenye kura peke iliyo kuwa inaweza kubadilisha uamuzi wa kamati hiyo, aliposema Ijumaa kuwa atapiga kura kumpitisha Kavanaugh, baada ya siku moja kabla kusema alikuwa hajafikia uamuzi.

Haiko wazi iwapo Warepublikan watapata kura za kutosha kwa ajili ya mteule wao baada ya mahojiano yaliyo kuwa na hisia za juu Alhamisi wakati Kavanaugh kwa hasira akikanusha tuhuma za kumbaka Ford katika tafrija mwaka 1982 wakati wakiwa vijana. Wote wawili walitoa maelezo yao kwa Kamati ya Sheria ya Baraza la Seneti katika mahojiano yaliyo chukua masaa tisa.

Alhamisi jioni, Seneta Bob Corker wa Jimbo la Tennessee alitangaza kuwa atampigia kura kuthibitisha Kavanaugh katika uteuzi huo wa Mahakama ya Juu. Wakati huohuo, amesema, ilikuwa ni ushujaa mkubwa kwa Ford kutoa ushahidi, kwani kulikuwa hakuna ushahidi wa kuthibitisha madai yake..

Seneta Jeff Flake wa Arizona amesema bado anafikiria namna ya kupiga kura baada ya kusikia maelezo ya Ford na Kavanaugh.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG