Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 12, 2025 Local time: 06:46

Kura ya kumpitisha Kavanaugh kufanyika Jumamosi


Wanaharakati wakiwa nje ya Mahakama ya Juu ya Marekani wakifanya maombi dhidi ya uteuzi wa Brett Kavanaugh katika mahakama hiyo, iliyofanyika Washington, Octoba 3, 2018.
Wanaharakati wakiwa nje ya Mahakama ya Juu ya Marekani wakifanya maombi dhidi ya uteuzi wa Brett Kavanaugh katika mahakama hiyo, iliyofanyika Washington, Octoba 3, 2018.

Uteuzi wa Jaji Brett Kavanaugh kujaza nafasi iliyo kuwa wazi katika Mahakama ya Juu Marekani unaelekea kwenye upigaji kura wa mwisho mapema siku ya Jumamosi.

Hata hivyo kitu cha kwanza, maseneta Alhamisi watapitia ripoti ya Idara ya Upelelezi ya Makosa ya Jinai FBI juu ya shutuma dhidi ya Kavanaugh kwamba alimnyanyasa kingono wakati wakiwa vijana na kuwa alimvulia nguo mwanamke mwengine wakati akiwa mwaka wa kwanza chuo kikuu.

Kwa upande wake Kavanaugh amekanusha tuhuma hizo.

Kile ambacho ni mvutano mkali wa mrengo wa kichama juu ya uteuzi wa maisha wa majaji tisa wa mahakama hiyo umeligawanya Baraza la Seneti la Marekani wakati Warepublikan walio wengi wakiwatuhumu Wademokrat kwa kuzorotesha mchakato huo wa uteuzi bila umuhimu wowote.

Nao Wademokrat wamesema Warepublikan wanaharakisha kumthibitisha Kavanaugh kuchukua nafasi hiyo bila ya kuzingatia vilivyo shutuma zilizo tolewa dhidi yake.

Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria Seneta Chuck Grassley amesema mapema Alhamisi jopo hilo lilipokea nyaraka za uchunguzi za FBI, na kuwa yeye na Seneta wa ngazi ya juu wa Demokrat Dianne Feinstein alikuwa amekubali mchakato wa pande zote kuchangia kwa zamu, ambao unatoa fursa sawa kwa pande zote mbili kutathmini taarifa hiyo.

XS
SM
MD
LG