Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:51

Saudi Arabia yasisitiza uamuzi wa kupunguza kiwango cha uzalishaji mafuta ni kwa sababu za kiuchumi


Rais wa Marekani Joe Biden (kushoto) na Prince Mohammed bin Salman
Rais wa Marekani Joe Biden (kushoto) na Prince Mohammed bin Salman

Saudi Arabia imekataa ukosoaji “usiokuwa na ukweli” wa uamuzi wa OPEC+ wiki iliyopita kupunguza kiwango cha uzalishaji mafuta licha ya Marekani kupinga hatua hiyo.

Saudi Arabia pia ilisema Alhamisi kuwa ombi la Washington kuchelewesha kupunguza uzalishaji huo kwa mwezi mmoja ungekuwa na matokeo mabaya ya kiuchumi.

Ikulu ya Marekani imelisukuma suala hilo, ikisema iliwasilisha kwa Saudi Arabia mchanganuo uliokuwa unaonyesha kupunguza uzalishaji kungeathiri uchumi wa dunia, na kudai kuwa Wasaudi waliwashinikiza wanachama wengine wa OPEC kupiga kura ya kupinga. Maafisa wa nchi zote mbili wanatarajiwa kujadili hali hiyo siku chache zijazo.

Hatua hii ya kujadiliana kufikia makubaliano imeongeza kile ambacho tayari kimezorotesha mahusiano ya nchi hizo mbili, ambazo zilikuwa na ushirikiano wa nishati kwa usalama kwa miongo kadhaa.

OPEC+, ni kikundi cha wazalishaji mafuta ikiwemo Jumuiya ya Nchi Zinazouza Mafuta (OPEC) pamoja na washirika wengine ikiwemo Russia, wiki iliyopita ilitangaza kupunguza uzalishaji kwa mapipa milioni 2 kwa siku katika kiwango walichojiwekea baada ya wiki kadhaa za maafisa wa Marekani kuwashawishi wasichukue hatua hiyo.

Machimbo ya mafuta ya Khurais kilomita 150 mashariki kaskazini mashariki ya Riyadh, Saudi Arabia.
Machimbo ya mafuta ya Khurais kilomita 150 mashariki kaskazini mashariki ya Riyadh, Saudi Arabia.

Hatua hiyo imekuja ingawaje soko la mafuta bado limebana, huku kiwango cha mafuta katika nchi zenye uchumi mkubwa zikiwa katika viwango vya chini kuliko ilivyokuwa huko nyuma wakati OPEC inapopunguza uzalishaji.

Upunguzaji wa uzalishaji uliofanywa na OPEC+ umeleta wasiwasi kwa Washington kuhusu uwezekano wa bei za mafuta kupanda zaidi kabla ya uchaguzi was katikati ya awamu nchini Marekani, huku Wademokrat wakijaribu kutaka kuendeleza kudhibiti Baraza la Wawakilishi na Baraza la Seneti.

Rais wa Marekani Joe Biden aliahidi mapema wiki hii kuwa “kutakuwa na athari” katika mahusiano ya Marekani na Saudi Arabia baada ya OPEC+ kuchukua hatua hii.

Alipoulizwa Alhamisi kuhusu hali hiyo wakati wa ziara yake huko Los Angeles, Biden aliwaambia waandishi wa habari “Tunakaribia kufanya mazungumzo nao.”

Uamuzi wa OPEC ulifikiwa kupitia maridhiano, ulizingatia uwiano wa usambazaji na mahitaji na ulikuwa na lengo la kuzuia kuyumba kwa soko la mafuta, wizara ya mambo ya nje ya Saudi Arabia ilieleza katika taarifa.

Taarifa ya Wizara ya mambo ya nje ya Saudi Arabia ilieleza mashauriano waliofanya na Marekani kabla ya mkutano wa OPEC+ wa Octoba 5 ambapo iliombwa kuchelewesha kupunguza uzalishaji kwa muda wa mwezi moja.

“Ufalme huo ulifafanua kupitia mashauriano endelevu na uongozi wa Marekani kuwa kila uchambuzi wa kiuchumi uliashiria kuwa kuchelewesha uamuzi wa OPEC+ kwa mwezi moja, kulingana na kile kilichopendekezwa kungekuwa na athari mbaya za kiuchumi,” wizara ya mambo ya nje ya Saudi Arabia ilisema.

FILE PHOTO: Rais wa Russia Vladimir Putin
FILE PHOTO: Rais wa Russia Vladimir Putin

Marekani iliishutumu Saudi Arabia kwa kuinyenyekea Moscow, ambayo inapinga kiwango cha bei iliyowekwa na nchi za Magharibi kwa mafuta ya Russia ikiwa ni hatua ya kukabiliana na uvamizi wa Russia nchini Ukraine.

“Tuliwasilisha kwa Saudi Arabia uchambuzi kuonyesha kuwa hakukuwa na msingi wowote wa kupunguza uzalishaji wa kiwango kilichowekwa, na ilikuwa rahisi kusubiri hadi mkutano mwengine wa OPEC kuona vipi hali itakavyokuwa,” msemaji wa White House Jack Kirby alisema, katika taarifa yake, ikiongeza kuwa nchi nyingine za OPEC waliiambia Marekani walikuwa wanahisi “walilazimishwa” kuunga mkono uamuzi wa Saudia.

Taarifa ya Wizara ya mambo ya nje ya Saudi Arabia, ikimnukuu afisa ambaye jina lake halikutajwa, ilisisitiza kuwa “kupunguza uzalishaji “kiuhalisia ilikuwa kwa sababu za kiuchumi”. Mahitaji ya mafuta yamekuwa chini duniani, huku OPEC, Wizara ya Nishati ya Marekani, na Shirika la Kimataifa la Nishati wakionyesha utabiri wa mahitaji ya mafuta yako chini mwaka 2023, wiki hii.

XS
SM
MD
LG