Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 10:59

Uhusiano kati ya Marekani na Saudi Arabia unaimarika


Rais Joe Biden akizungumzia uwezekano wa kuitembelea Saudi Arabia
Rais Joe Biden akizungumzia uwezekano wa kuitembelea Saudi Arabia

Kulingana na maafisa wa serikali, ujumbe wa kwanza wa Saudi Arabia utaitembelea Washington tarehe 15 Juni na utaongozwa na waziri wa biashara Majid bin Abdullah al-Qasabi.

Ujumbe wa pili utaongozwa na waziri wa uwekezaji Khaled Al-Falih umepangwa kuwasili mwishoni mwa mwezi huu na utawajumuisha maafisa wa serikali na wafanyabiashara.

Kulingana na maafisa wa Marekani wanaofahamu zaidi juu ya ziara hizo, wanasema mazungumzo ya wajumbe hao yatazingatia juu ya makubaliano na mikataba kuhusiana na sekta mbali mbali, ikiwa ni pamoja na usafiri, uchukuzi, na nishati mbadala.

Rais Biden alikiri hadharani siku ya Ijumaa kwamba huenda akaitembelea Saudi Arabia hivi karibuni, ziara ambayo maafisa kadhaa wamethibitisha na huenda pia akazungumza na mwana mfalme Mohammed bin Salman.

Ziara hiyo itasaidia kurekebisha uhusiano na Saudi Arabia, ambao umekuwa na mivutano kwasababu ya kupanda kwa bei za mafuta, vita vya Yemen na kuuawa kwa mwandishi wa habari Jamal Khashoggi raia wa Saudia mwaka 2018 katika ubalozi mdogo wa ufalme huo mjini Istanbul.

XS
SM
MD
LG