Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 01, 2023 Local time: 06:07

Biden: Marekani itaendelea kujihusisha kwa dhati Mashariki ya Kati


Rais Joe Biden wa Marekani akikutana na viongozi wa nchi za Kiarabu kujadili usalama na maendeleo.
Rais Joe Biden wa Marekani akikutana na viongozi wa nchi za Kiarabu kujadili usalama na maendeleo.

Rais Joe Biden wa Marekani amemaliza ziara ya siku nne Mashariki ya Kati ambako amewahakikishia viongozi wa nchi za kiarabu kwamba Marekani itaendelea kujihusisha kwa dhati Mashariki ya Kati.

Katika mkutano mjini Jeddah, Saudi Arabia uliongozwa na mwana mfalme Mohammed bin Salman, pamoja na viongozi wa nchi 6 wa Baraza la Ushirikiano wa nchi za Ghuba, GCC, na Misri, Jordan na Iraq, Rais Biden amesema "Marekani haitaondoka kutoka kanda hiyo na kuacha nafasi kuchukuliwa na China, Rashia au Iran."

Biden amekua akijaribu katika ziara yake ya kwanza ya Mashariki ya Kati tangu kuchukua madaraka mwezi Januari mwaka 2021, kuzungumzia namna ya kuzuia kupanda kwabei za mafuta na kueleza mawazo na mikakati ya Washington katika kanda zima.

Taarifa baada ya mkutano haikueleza bayana matokeo yaliyopatikana, lakini inaonekana Biden hakufaulu kupata uhakikisho kutoka kwa viongozi wenzake wa nchi za kiarabu juu ya kuongeza uzalishaji mafuta wala kuitisha mkutano wa viongozi juu ya kuunda mungano utakaoihusisha Israel, wa kupambana na vitisho vya Iran.

Wakati wa mkutano wa ana kwa ana na mwana mfalme Mohammed, Biden anasema walizungumzia masuala nyeti kuhusu haki za binadamu, kuondoa ukosoaji dhidi ya mwana mfalme na ushirikiano kati ya nchi zao mbili.

Siku ya Ijumaa Rais Biden pamoja na mwana mfalme Mohammed walishuhudia kutiwa saini mikataba 18 kati ya nchi zao mbili kuhusiana na ushirikiano wa nishati, anga za juu, afya na uwekezaji.

Biden pia ameahidi dola bilioni moja ya msaada wa chakula kwa nchi za Mashariki ya Kati.

XS
SM
MD
LG