Upatikanaji viungo

Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 21:14

Ethiopia yaanza kuwarejesha raia wake walio Saudi Arabia

watoto wa Ethiopia wanaosafirishwa kutoka Saudi Arabia wakisubiri kuandikishwa baada ya kushuka kutoka kwa ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole mjini Addis Ababa, Ethiopia, April 1 2022 PICHA: REUTERS

Ethiopia imewasafirisha watoto 101 kutoka Saudi Arabia hii leo wakati inaendelea na kampeni yake ya kuwarudisha maelfu ya raia wake kutoka taifa hilo.

Idadi kubwa ya raia wa Ethiopia walio katika nchi hiyo ya mashariki ya kati hawana vibali vya uhamiaji na wanazuiliwa katika mazingira mabaya.

Kulingana na wizara inayoshughulikia maswala ya wanawake na mambo ya kijamii, karibu wahamiaji 5000 wamerudishwa Ethiopia tangu shughuli hiyo ilipoanza zaidi ya wiki moja iliyopita.

Maafisa wa serikali wamesema kwamba shughuli hiyo huenda ikachukua mda wa miezi 11 na inalenga kuwarudisha nyumbani raia wa Ethiopia 100,000 kutoka Saudi Arabia.

XS
SM
MD
LG