Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 23:37

Rwanda yasimamisha safari za ndege kwenda Kusini mwa Afrika


Rwanda yasitisha safari zake za ndege Kusini mwa Afrika
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:04 0:00

Rwanda yasitisha safari zake za ndege Kusini mwa Afrika

Rwanda imesimaisha kwa muda safari zake za ndege kati ya Rwanda na nchi za Kusini mwa Afrika kufuatia maambukizo ya aina mpya ya kirusi kipya cha COVID-19 Omicron.

Nchi hiyo pia imeweka masharti ya kujiweka KARANTINI kwa siku saba kwa wasafiri wote wanaowasili Kigali ambao hivi karibuni walikuwa katika nchi zilizoathiriwa na corona.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, Rwanda inafanya haya kwa ajili ya kudhibiti maambukizo ya kirusi kipya kilichogunduliwa Afrika Kusini na nchi jirani wiki iliyopita na kutangazwa Novemba 25.

Kirusi cha Omicron tayari kimethibitishwa katika nchi 13. Maamuzi hayo yalifanyika baada ya kikao cha dharura cha Baraza la Mawaziri Jumapili kilichokuwa kinajadili jinsi ya kupambana na kirusi hicho.

Kikao hicho kiliongozwa na Rais Paul Kagame. Rwanda inaungana na Umoja wa Ulaya, Marekani, Israeli, nchi za Jumuiya ya Kiarabu, Uingereza miongoni mwa nchi nyingine ambazo zimesimamisha safari zake kwenda kusini mwa AFrika.

XS
SM
MD
LG