Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 05, 2022 Local time: 13:57

Maambukizi mapya ya aina mpya ya virusi yagunduliwa Uholanzi, Australia


Watu wakitembea ndani ya uwanja wa ndege Schiphol baada ya mamlaka ya afya Uholanzi kusema watu 61 waliowasili Amsterdam na ndege ya Afrika Kusini walikutikana na maambukizi ya COVID-19, Amsterdam, Netherlands, Nov. 27, 2021. REUTERS/Eva Plevier

Maafisa wa afya Uhalonzi wamesema Jumapili watu 13 ambao hivi karibuni waliwasili nchini  Uholanzi katika ndege iliyokuwa inatokea Afrika Kusini wamegundulika wana maambukizi ya aina mpya ya virusi vya omicron.

Abiria hao walikuwa sehemu ya kikundi cha watu 61 waliogundulika na maambukizi ya virusi vya corona baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Amsterdam Ijumaa.

Tangazo hilo limekuja muda mfupi baada ya Australia kusema kesi mbili za aina mpya za virusi zimegunduliwa kwa wasafiri waliokuwa wamewasili Sydney hivi karibuni.

Omicron ni aina ya tano iliyokuwa imetangazwa na WHO inayo tishia. Mara ya kwanza iligundulika katika wiki za karibuni Afrika Kusini, ambayo imeonyesha kuongezeka kwa maambukizi ya COVID-19 kwa haraka sana.

Kuna aina 30 za mabadiliko katika protini ya virusi vinavyoshambulia, na wanasayansi wana wasiwasi kuwa baadhi yake vinaweza kuviwezesha virusi kuambukiza kwa urahisi. Lakini wana sayansi bado hawajajua iwapo omicron kwa hakika inaambukiza zaidi au hatari zaidi.

Maambukizi ya aina mpya ya virusi pia vimegunduliwa nchini Israeli, Hong Kong na nchi kadhaa za Ulaya.

Wasiwasi juu ya aina mpya ya virusi vimesababisha nchi nyingi, ikiwemo Marekani, Canada na mataifa ya Umoja wa Ulaya, kuweka masharti au kupiga marufuku wasafiri kutoka nchi za Kusini mwa Afrika.

Abiria wakisubiri Majibu ya kipimo cha COVID-19 uwanja wa ndege wa Schiphol, Amsterdam, Netherlands ,MEDIA PHOTO OBTAINED BY REUTERS/
Abiria wakisubiri Majibu ya kipimo cha COVID-19 uwanja wa ndege wa Schiphol, Amsterdam, Netherlands ,MEDIA PHOTO OBTAINED BY REUTERS/

Serikali ya Afrika Kusini imesema masharti ya kusafiri “yameharakishwa” na kuelezea wasi wasi wao juu ya athari zake kwa biashara.

Mtaalam wa ngazi ya juu wa Marekani wa magonjwa ya kuambukiza, Dkt Anthony Fauci, amesema hatoshangaa iwapo aina mpya ya virusi omicron iko pia tayari nchini Marekani.

Nchini Afrika Kusini, ambako aina mpya iligundulika, kiasi cha asilimia 35 ya watu wazima wamechanjwa. Idadi ya waliochanjwa ni ndogo katika nchi nyingi barani Afrika.

Wataalam wa afya wametahadharisha kutokuwepo uwiano wa chanjo kunaweza kuleta kuzaliana kwa aina mpya ya virusi.

Vyanzo vya habari hii inatokana na mashirika la habari la AP na Reuters.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG