Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 01:52

Morocco kusitisha safari za ndege kutokana na virusi vipya


Waziri wa mambo ya nje wa Morocco Nasser Bourita .

Wizara ya mambo ya nje  ya Morocco imesema Jumapili kwamba kuanzia leo Jumatatu itasitisha safari za ndege kuingia nchini  humo kwa muda wa wiki mbili.

Hatua hiyo ni kutokana na aina mpya ya virusi vya corona vya Omicron. Kwa mijibu wa shirika la habari la AP, wizara hiyo kupitia ujumbe wa twitter imesema kwamba hatua hiyo ni ya kuhakikisha mafanikio yaliyopatikana katika mapambano dhidi ya janga hilo na kulinda afya za raia wake.

Mwaka uliopita Morocco ilifunga mipaka yake kwa miezi kadhaa baada ya kutokea kwa janga hilo kwa kuhofia kwamba mfumo wake wa afya usingeweza kukabiliana na janga hilo kama ilivyokuwa likishuhudiwa kwenye mataifa kadhaa ya Ulaya.

Taifa hilo hata hivyo ni miongoni mwa yale yaliyojitahidi kutoa chanjo kwa watu wake huku asilimia 66 tayari wakiwa wamepokea walau dozi moja. Hatua ya kufungwa kwa safari za ndege pia imechukuliwa na mataifa mengine mengi kote ulimwenguni ikiwa kama hatua ya kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo vipya ambavyo kwa mara ya kwanza vilitangazwa Afrika kusini.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG