Kigali na Kinshasa zimekuwa zikilaumiana kwa kuzuka upya kwa mapigano na ukosefu wa utulivu mashariki mwa Kongo, ambapo waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wameuteka mji mkuu wa eneo hilo na wanasonga mbele katika maeneo zaidi, huku mamia wakiuawa na maelfu kufurushwa makwao
"Tunapinga vikali shuruma za DRC dhidi ya Rwanda kwa kuhusika katika kusababisha ukosefu wa utulivu mashariki mwa DRC," mwakilishi wa Rwanda katika Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Uswizi, James Ngango, aliambia mkutano wa dharura wa Baraza la Haki za Kibinadamu.
"Kilicho wazi, hata hivyo, ni tishio kwa Rwanda linalosababishwa na hali inayoendelea hivi sasa. Kufuatia kuanguka kwa Goma, ushahidi mpya umepatikana kuhusiana na shambulio kubwa linalopangwa dhidi ya Rwanda," alisema na kuongeza kuwa Kinshasa na washirika wake walikuwa wamehifadhi silaha ndani na karibu na uwanja wa ndege wa Goma. Hadi tulipokuwa tukiandaa ripoti hii, hakukuwa na majibu ya moja kwa moja kutoka kwa maafisa wa serikali ya DRC.
Forum