"Wataambukizwa kabla hatujawatibu wote," alisema Florence Douet, muuguzi wa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Bethesda, alipokuwa akihudumia wagonjwa wenye viwango tofauti vya majeraha.
Tangu kuanza kwa mashambulizi ya waasi wa M23 huko Goma tarehe 26 mwezi Januari mwaka huu, zaidi ya watu 700 wameuawa na karibu 3,000 wamejeruhiwa katika mji huo na viunga vyake, maafisa wanasema.
Hospitali ya Bethesda pekee ilisema inapokea zaidi ya wagonjwa wapya 100 kila siku, na kuzidi uwezo wake, ikiwa na vitanda 250.
Bethesda ni mojawapo ya hospitali kadhaa huko Goma ambazo shirika la habari la Associated Press lilitembelea ambayo haina wafanyikazi na vifaa vya kutosha.
Jiji hilo linatoa hifadhi kwa takriban watu milioni 6.5 waliokimbia makazi yao kutokana na mzozo huo, ambao ni mojawapo ya majanga makubwa zaidi ya kibinadamu duniani.
Forum