Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Agosti 19, 2022 Local time: 13:24

Russia yadai zaidi ya wanajeshi 1,000 wa Ukraine wamejisalimisha Mariupol


Picha za satellite zinaonyesha majengo yakiteketea Mariupol (Picha na Reuters).

Taarifa hii ni kufuatia mkakati wake mkubwa wa kuulenga  mkoa wa Donbas mashariki mwa nchi,  ambao umeharibiwa vibaya lakini bado hauko chini ya udhibiti wa Russia.

Zaidi ya wanajeshi 1,000 wa Ukraine wamejisalimisha katika mji wa bandari wa Mariupol, Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema Jumatano.

Taarifa hii ni kufuatia mkakati wake mkubwa wa kuulenga mkoa wa Donbas mashariki mwa nchi, ambao umeharibiwa vibaya lakini bado hauko chini ya udhibiti wa Russia.

Kama Russia itachukua wilaya ya viwanda ya Azovstal ambako wanajeshi hao wamezingirwa watakuwa wanadhibiti kikamilifu Mariupol, bandari kuu ya Ukraine ya bahari ya Azov.

Hilo litairuhusu Russia kuimarisha ukanda wa ardhini kati ya maeneo ya mashariki yanayoshikiliwa na watu wanaojitenga na eneo la Crimea ambalo ililikamata na kujiingiza huko mwaka 2014.

Ukiwa umezingirwa na kushambuliwa na wanajeshi wa Russia kwa wiki kadhaa na mwelekeo wa baadhi ya mapigano makali zaidi ya vita hivyo.

Mariupol ungekuwa mji wa kwanza mkubwa kuanguka tangu Russia ilipoivamia Ukraine mwezi Februari.

Wizara ya ulinzi ilisema wanajeshi hao 1,026 wamejisalimisha ikiwemo maafisa wengine 162.

Generali wa Ukraine amesema kwamba Russia inaendelea na mashambulizi dhidi ya Azovstal na bandari lakini msemaji wa wizara ya ulinzi alisema hana taarifa yoyote kuhusu kujisalimisha.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG