Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 11:02

Uingereza yatangaza vikwazzo kadhaa dhidi ya wafadhili wa vita vya Ukraine


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akihutubia bunge la Uingereza kwa njia ya video, March 8 2022. Kiongozi huyo wa Ukraine aliomba Uingereza kuongeza vikwazo dhidi ya wafadhili wa vita vya Ukraine
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akihutubia bunge la Uingereza kwa njia ya video, March 8 2022. Kiongozi huyo wa Ukraine aliomba Uingereza kuongeza vikwazo dhidi ya wafadhili wa vita vya Ukraine

Uingereza imesema kwamba imewawekea vikwazo watu 206 kutokana na uvamizi wa Russia nchini Ukraine, wakiwemo 178 ambao imesema waliunga mkono hatua ya Russia kujinyakulia sehemu za Ukraine.

Ofisi ya mambo ya nje ya Uingereza imesema kwamba kati ya waliowekewa vikwazo hivyo ni Alexander Ananchenko na Sergey Kozlov, ambao imewataja kuwa watu waliojitangaza kuwa waziri mkuu na mwenyekiti wa serikali zinazojiita Donetsk na jamhuri ya watu wa Luhansk.

Wengine waliowekewa vikwazo ni watu kutoka familia ya maafisa wa ngazi ya juu katika serikali ya Russia, wakiwemo Pavel Ezubov, ambaye ni ndugu wa bilionea wa Russia Oleg Deripaska, na Nigina Zairova, ambaye ni msaidizi mkuu wa mfanyabiashara Mikhail Fridman.

Mke wa waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergey Lavrov, Maria Lavrova, amewekewa vikwazo vya kutosafiri, pamoja na mali zake.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Liz Truss amesema kwamba wataendelea kuwawekea vikwazo watuw anaofanikisha vita vya Russia dhidi ya Ukraine.

Serikali ya Uingereza vile vile imetangaza kwamba itapiga marufuku uagizaji wa bidhaa za chuma kutoka Russia.

XS
SM
MD
LG