Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 11:59

Ripoti ya CAG yaonyesha mashirika ya umma yanauhaba wa fedha


Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mussa Assad akiwa na timu yake ya wakaguzi na Rais Magufuli, Waziri Mkuu Majaliwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu, Januari 2019.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mussa Assad akiwa na timu yake ya wakaguzi na Rais Magufuli, Waziri Mkuu Majaliwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu, Januari 2019.

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali nchini Tanzania (CAG), Mussa Assad ya mwaka wa fedha 2017/2018 imebainisha mashirika ya umma yana hali mbaya ya uhaba wa fedha.

Ripoti hiyo iliyowasilishwa Jumatano bungeni mjini Dodoma, pia imebainisha matumizi mabaya ya fedha kwa vyama vya siasa na kudai kuwa katika ripoti iliyopita ni mapendekezo 80 pekee kati ya 350 yaliyofanyiwa kazi kikamilifu.

Prof Assad alieleza: "Hatujakurupuka kufanya mkutano huu hapa ofisini kwetu. Tulihisi mapema hatutakaribishwa bungeni. Tumeongea nanyi hapa kwetu, hata kama ninyi waandishi wa habari hamtatoa hiki tulichozungumza, sisi tutatoa kwa umma."

CAG amesisitiza kuwa neno 'dhaifu' ni lugha ya kawaida katika ukaguzi wetu. na litaendelea kutumika.

Mahojiano maalum na CAG

Tanzania : Profesa Assad aeleza kwa nini deni la taifa bado himilivu
please wait

No media source currently available

0:00 0:07:46 0:00


Miaka iliyopita, CAG alikuwa anatoa mukhtasari huo kwa waandishi wa habari bungeni mara tu baada ya ripoti yake kuwasilishwa kwenye chombo hicho.

Wakati anazungumza na waandishi Profesa Assad aliwaambia kuwa "nimetazama kwenye TV ripoti imewasilishwa bungeni na 'order paper' (karatasi yenye orodha ya shughuli za kikao cha Bunge) ninayo hapa inaonyesha ripoti imekabidhiwa bungeni Jumatano, asubuhi, na nimetazama ikiwasilishwa.

Pia amesema mwaka 2019 ofisi yake imetoa ripoti yake kwa CD ili kuepuka gharama nyingi za uchapishaji.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG