Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 17, 2024 Local time: 19:13

Rais Zelenskyy: Washirika waharakishe upelekaji silaha walizo iahidi Ukraine


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy

Mashambulizi ya Russia huko kusini mwa Ukraine katika  mji wa  Kherson Jumapili yameua watu watatu na kujeruhi wengine sita.

Mashambulizi yalimsukuma Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, kwa mara nyingine, kuelezea umuhimu kwa washirika kuharakisha upelekaji wa silaha walizoahidi kuzituma.

“Inabidi tufikishiwe silaha zetu kwa wakati,” rais alisema katika hotuba ya kila siku. “Ni lazima … tuharakishe kupeleka na kutoa fursa mpya muhimu kwa silaha kwa ajili ya Ukraine.

Zelenskyy pia alisema kuwa majengo ya makazi, hospitali, shule, kituo cha basi, ofisi ya posta na benki ni kati ya vitu vilivyoharibiwa katika mashambulizi ya Kherson.

Russia na Ukraine zilitoa madai yanayokinzana siku ya Jumapili juu ya nani anadhibiti eneo karibu na Blahodatne upande wa mashariki wa mkoa wa Donetsk.

Kikundi cha mamluki wa kijeshi cha Wagner cha Russia kimedai kuchukuaudhibiti wa kijiji, wakati jeshi la Ukraine likisema vikosi vyake vilizima mashambulizi.

“Vikosi vya Jeshi la Ulinzi la Ukraine vilizima mashambulizi ya wavamizi katika maeneo ya … Blahodatne … katika mkoa wa Donetsk,” Mkuu wa Wafanyakazi wa Jeshi la Ukraine alisema katika ripoti yake ya kila siku asubuhi, akielezea mapigano ya Jumamosi.

Ukraine ilisema vikosi vyake pia vimezuia mashambulizi ya Russia katika maeneo ya makazi takriban 13 katika mkoa wa Donetsk.

Lakini Kikundi cha Wagner, kilichotanjwa na Marekani kama ni taasisi ya kimataifa ya uhalifu, kilisema katika ujumbe wake wa Telegram Jumamosi kuwa vikosi vyake vilichukuaudhibiti wa Blahodatne.

Shirika la Habari la Ufaransa limeripoti hakuna uthibitisho wa mara moja kutoka wizara ya ulinzi ya Russia.

XS
SM
MD
LG