Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 00:46

Russia yaanzisha mashambulizi mapya ya makombora, wakati Marekani na Ujerumani zikiahidi kupeleka vifaru vya kisasa Ukraine


Watu wamekusanyika katika kituo cha treni ya ardhini kinachotumika kujihifadhi na mashambulizi ya mabomu na roketi yanayofanywa na Russia dhidi ya mji wa Kyiv, Ukraine, Jan 26, 2023.
Watu wamekusanyika katika kituo cha treni ya ardhini kinachotumika kujihifadhi na mashambulizi ya mabomu na roketi yanayofanywa na Russia dhidi ya mji wa Kyiv, Ukraine, Jan 26, 2023.

Russia imefanya  wimbi jipya la mashambulizi ya makombora kwa Ukraine Alhamisi Asubuhi, na kuua mtu moja, saa kadhaa baada ya shambulizi la ndege isiyo na rubani  usiku.

Wakati huo huo mapigano makali yanaendelea bila ya kusitishwa upande wa mashariki, ambako majeshi ya Moscow yamekuwa yakiweka shinikizo kwa jeshi la Ukraine.

Mashambulizi mapya ya makombora yamekuja baada ya Rais Volodymyr Zelenskyy, kuongea saa chache baada ya Ujerumani na Marekani kuahidi kuipatia Kyiv vifaru vya kisasa vya vita, kufuatia wito wa Kyiv kwa washirika wake wa Magharibi kutuma makombora ya masafa marefu na ndege za kivita kuimarisha ulinzi wa anga wa Ukraine.

Meya wa Kyiv Vitali Klitschko alisema mtu mmoja aliuawa na wengine wawili kujeruhiwa katika shambulizi kwenye mji mkuu na kuwasihi wakaazi wake kuhamia mafichoni.

“Ikiwa ni matokeo ya shambulizi la roketi katika jengo la kawaida lisilokaliwa na watu huko wilaya ya Holosiyiv, tuna habari kuwa mtu mmoja ameuawa na wengine wawili wamejeruhiwa. Majeruhi hao wamelazwa hospitali,” alisema.

Serhiy Popko, mkuu wa uongozi wa kijeshi mjini Kyiv, alisema zaidi ya darzeni za makombora yaliharibiwa na mfumo wa ulinzi wa anga.

“Adui huyo alikuwa ametuma zaidi ya makombora 15 kuelekea Kyiv. Shukran kwa kazi nzuri sana ya ulinzi wa anga, makombora yote yaliyolengwa yalitunguliwa,” alisema.

Andriy Yermak, mkuu wa utawala katika ofisi ya rais wa Ukraine, aliandika katika ujumbe wa Telegram “makombora ya kwanza ya Russia yametunguliwa,” bila ya kutaja maeneo ambako yalitunguliwa.

Vituo viwili vya nishati vilishambuliwa na makombora ya Russia katika mkoa wa kusini wa Odesa, mamlaka katika eneo zilisema.

Baadhi ya taarifa katika ripoti hii zinatokana na mashirika ya habari ya Reuters, AP na AFP na dpa.

XS
SM
MD
LG