Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 23, 2023 Local time: 02:07

Mashambulizi ya makombora ya Russia yaua watu 11 nchini Ukraine


Majengo yaharibiwa na mashambulizi ya makombora ya Russia

Russia ilifanya mashambulizi ya makombora kwenye maeneo tofauti nchini Ukraine Jana Alhamisi ambayo yaliua watu 11 na kujeruhi wengine 11, maafisa wameripoti.

Idara ya huduma za dharura ya Ukraine imesema mashambulizi hayo yalilenga maeneo 11 nchini kote. Jeshi la anga la Ukraine limesema Russia ilifyatua makombora 55, huku Ukraine ikitungua mengi kati ya hayo. Majengo 35 yaliharibika katika mashambulizi hayo.

Vikosi vya Moscow vimeendelea kulenga miundombinu ya nishati ya Ukraine wakati wa kipindi cha msimu wa baridi, katika juhudi za kuwavunja moyo Waukraine.

Waziri mkuu wa Ukraine Denys Shmyal amesema katika taarifa kwenye Telegram, “Lengo lao kuu ni vituo vya nishati, vinavyosambaza umeme na joto ndani ya nyumba.”

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG