Duru za habari za kuaminika nchini Morocco zinasema kuwa Rais Azali alipelekwa hospitali kutoka uwanja wa ndege akiwa hajihisi vizuri na hakuna taarifa juu ya hali yake iliyotolewa rasmi na maafisa wa Comoro au Moroco.
Wiki mbili zilizopita kiongozi huyo alianguka na kupoteza fahamu alipokuwa akihutubia sherehe za kuadhimisha miaka 15 tangu kuanzishwa kwa chuo kikuu cha Comoro na ripoti zisizo thibitishwa zinaeleza kwamba alipatwa na kiharusi.
Habari hizo zinatokea wakati mahakama moja ya Moroni imemhukumu makamu rais wa zamani Jaffar Said Ahmed aliyeko uhamishoni nchini Tanzania kifungo cha maisha na kazi ngumu.
Mahakama hiyo pia imetoa huku kama hiyo kwa mkuu wa zamani wa jeshi Kanali Ibrahim Salim na kaka yake Makamu Rais na mwandishi wa habari kwa kupanga njama ya kujaribu kuipindua serikali ya Moroni.