Hii inakuja siku kadhaa baada ya mapinduzi ya kijeshi ambayo yameshutumiwa vikali na jumuiya ya kimataifa.
Kabore anashikiliwa katika makazi ya rais kwenye kifungo cha nyumbani, yuko salama kimwili na anaye daktari anayemwangalia, hiyo ni kwa mujibu wa mwanachama wa juu wa chama chake cha MPP.
Kwa saa kadhaa siku ya Jumatatu hatma ya mapinduzi ya rais haikueleweka kukiwa na taarifa zenye kutatanisha zilizoenea kuhusu kukamatwa kwake au hata jaribio la kuuawa.
Mkutano usio wa kawaida wa ECOWAS utafanyika ijumaa kujadili hali ilivyo huko Burkina Faso baada ya Kabore kupinduliwa kukiwa na uwezekano wa kuwekwa vikwazo dhidi ya jeshi.