Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 25, 2025 Local time: 08:09

Putin afanya ziara kwenye makao makuu ya vikosi vya Russia vilivyoko nchini Ukraine

Rais wa Russia Vladimir Putin azuru makao makuu yenye mkusanyiko wa majeshi ya Dniepr katika mkoa wa Kherson nchini Ukraine, ambao majeshi ya Russia yanadhibiti baadhi ya maeneo. (Picha na AFP).
Rais wa Russia Vladimir Putin azuru makao makuu yenye mkusanyiko wa majeshi ya Dniepr katika mkoa wa Kherson nchini Ukraine, ambao majeshi ya Russia yanadhibiti baadhi ya maeneo. (Picha na AFP).

Kremlin imesema Jumanne kwamba Rais wa Russia Vladmir Putin alitembelea makao makuu ya vikosi vya Russia huko Ukraine.

Picha ya video iliyotolewa mapema Jumanne imemuonyesha Putin akiwa anatembelea kituo cha kijeshi katika Mkoa wa Kusini wa Kherson.

Picha zimemuonyesha rais huyo akipokea taarifa kutoka kwa viongozi waandamizi wa kijeshi.

Baadae aliondoka kwa helikopta hadi makao makuu ya jeshi la ulinzi la Russia katika mkoa wa Luhansk. Hii ni safari ya pili ya Putin katika maeneo hayo baada ya miezi mingi.

Rais wa Russia atembelea mkoa wa Kherson na kufanya mazungumzo na viongozi wa eneo hilo, Aprili 18, 2023. Kremlin.ru/Handout via REUTERS ATTENTION EDITORS -
Rais wa Russia atembelea mkoa wa Kherson na kufanya mazungumzo na viongozi wa eneo hilo, Aprili 18, 2023. Kremlin.ru/Handout via REUTERS ATTENTION EDITORS -

Putin alikutana na makamanda katika majimbo mawili ya Ukraine ambayo Moscow inadai kuyachukua, wakati vikosi vya Russia vikiendelea na upigaji mabomu na mashambulizi ya anga katika eneo lenye hali ngumu mashariki mwa Ukraine katika mji wa Bakhmut.

Hata hivyo msaidizi mkuu wa Rais wa Ukraine Mykhailo Podolyak alitumia mtandao wa Twitter kukejeli safari ya Putin kama” safari maalum ya mwandishi wa mauaji makubwa ya watu wengi katika maeneo yaliyochukuliwa na kuharibu vitongoji, kwa ajili ya kufurahia uhalifu wa marafiki zake kwa mara ya mwisho, “

Kyiv na nchi za Magharibi zinavishutumu vikosi vya Russia kwa kufanya uhalifu wa vita kwenye maeneo ya Ukraine yanayokaliwa kimabavu jambo ambalo Moscow inakanusha.

XS
SM
MD
LG