Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 23:49

Russia yaomba kuondolewa vikwazo ili kuruhusu tena usafirishaji wa nafaka ya Ukraine


Meli ya mizigo yakaguliwa kabla ya kusafirisha nafaka ya Ukraine , Agosti 3, 2022.

Russia Alhamisi imesema hakutakuwa na kuongeza muda kwa makubaliano yaliyosimamiwa na Umoja wa Mataifa ya kusafirisha nafaka za Ukraine kutoka bahari ya Black Sea baada ya tarehe 18 Mei, isipokuwa tu nchi za magharibi zikiondoa msururu wa vikwazo kwa mauzo ya nje ya nafaka na mbolea za Russia.

Makubaliano ya kusafirisha nafaka ya Ukraine yalisimamiwa na Umoja wa Mataifa na Uturuki mwezi Julai mwaka jana ili kusaidia kupunguza mzozo wa chakula duniani uliozidi kuwa mbaya kutokana na mzozo unaodumaza mauzo ya nje kutoka nchi hizo mbili ambazo ni wazilishishaji wakubwa wa nafaka duniani.

“Bila kupiga hatua kwa kutatua matatizo matano ya kimfumo, hakuna haja ya kuzungumza juu ya kuongeza muda zaidi kwa mpango wa kusafirisha nafaka kutoka Black Sea baada ya Mei 18,” wizara ya mambo ya nje ya Russia ilisema katika taarifa.

Wizara hiyo imeongeza kuwa “ Tulibaini kuwa licha ya taarifa zote za ngazi ya juu kuhusu usalama wa chakula duniani na msaada kwa nchi zenye mahitaji makubwa, mpango huo wa kusafirisha nafaka kutoka Black Sea ulinufaisha na unaendelea kunufaisha mauzo ya biashara ya Kyiv pekee kwa maslahi ya nchi za magharibi.”

Ili kusaidia kuishawishi Russia kuiruhusu Ukraine kuanza kusafirisha tena nafaka yake kutoka bandari yake ya Black Sea mwaka jana, makubaliano tofauti ya miaka mitatu yalifikiwa pia mwezi Julai ambapo Umoja wa mataifa ulikubali kuisaidia Russia kuuza nje chakula na mbolea zake.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema majadiliano, mawasiliano bado yanaendelea na pande zote, na maafisa wa Umoja wa Mataifa wana dhamira kuhakikisha utekelezaji wa makubaliano yote mawili.

XS
SM
MD
LG