Waandamanaji kwa siku nne mfululizo waliandamana mjini Ougadougu kupinga uwamuzi wa serikali kutaka kubadili katiba ili kumruhusu Rais Blaise Compaore kugombania tena kiti cha rais baada ya miaka 27 ya kuwa madarakani.
Waandamanaji walitia moto jengo la bunge Burkina Faso

1
Wanajeshi wajaribu kuwazuwia waandamanaji wanaoipinga serikali kuingia katika jengo la bunge mjini Ouagadougou, mji mkuu wa Burkina Faso, Oct. 30, 2014.

2
Mpinzani wa serikali akikabiliana na mwanajeshi nje ya jengo la bunge la taifa mjin Ouagadougou, mji mkuu wa Burkina Faso, Oct. 30, 2014.

3
Waandamanaji wafanikiwa kuingia ndani ya jengo la bunge na kulitia moto mjini Ouagadougou, Burkina Faso, Oct. 30, 2014.

4
Waandamanaji wasimama nje ya jengo la bunge linapowaka moto pamoja na magari na hati zilizokuwa nje ya jengo, mjini Ouagadougou, Burkina Faso, Oct. 30, 2014.