Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Agosti 15, 2022 Local time: 03:21

Polisi : Miili 39 yakutikana katika gari la mizigo Uingereza


Uingereza

Miili ya watu 39 imekutwa katika gari kubwa la mizigo ndani ya konteina moja nchini Uingereza.

Polisi wa Uingereza wanasema gari hilo kubwa la mizigo lilikutwa katika eneo la viwanda la Waterglade huko Grays ambako ni kiasi cha kilometa 32 mashariki ya London.

Taarifa hizo zimeeleza kuwa miongoni mwa waliokufa kuna watu wazima 38 na kijana mmoja.

Wachunguzi wanaamini kuwa gari hilo lilisafiri kutoka Bulgaria na kuingia Uingereza kupitia mji wa Holyhead huko Wales mwishoni mwa juma lililopita .

Mtu mmoja mwenye umri wa miaka 25 ambaye ametambuliwa kama dereva wa gari hilo ametiwa mbaroni kwa shutuma za mauaji.

Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametoa taarifa akisema amesikitishwa na janga hili kubwa.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG